Kafulila azungumzia mkatati wa rufaa matibabu ya nje

DAR ES SALAAM: Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP-Centre), David Kafulila, ameongoza kongamano la kitaifa kujadili mageuzi makubwa ya sekta ya afya, akibainisha kuwa uwekezaji unaofanywa sasa utamaliza kabisa adha ya kusafirisha wagonjwa nje ya nchi. Kongamano hilo limefanyika leo Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

DAR ES SALAAM: Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP-Centre), David Kafulila, ameongoza kongamano la kitaifa kujadili mageuzi makubwa ya sekta ya afya, akibainisha kuwa uwekezaji unaofanywa sasa utamaliza kabisa adha ya kusafirisha wagonjwa nje ya nchi.

Kongamano hilo limefanyika leo Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) jijini Dar es Salaam, likiwakutanisha wadau mbalimbali wa afya na uwekezaji kujadili nafasi ya ubia (PPP) katika utoaji wa huduma.

Kafulila alisema kuwa Serikali inaendelea kufanya uwekezaji mkubwa na wa kimkakati katika sekta ya afya ili kuboresha upatikanaji wa huduma za kiwango cha juu ndani ya nchi.

Aidha, alisisitiza kuwa uwekezaji huo kupitia ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) si tu kwamba unaleta huduma za kibingwa karibu na wananchi, bali unachukua nafasi kubwa katika kupunguza gharama za matibabu na kuongeza ufanisi wa mfumo mzima wa afya nchini, jambo litakalohakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora bila kuvuka mipaka.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports