Kihongosi: Tuwapinge wanaohamasisha chokochoko – HabariLeo

ARUSHA: Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi, amewataka Watanzania kuendelea kulinda uhuru, amani na utulivu wa nchi kwa kupinga hadharani watu wanaohamasisha chokochoko na vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa taifa. Kihongosi ameeleza hayo leo Juni 6,2026 alipotembelea na kuzindua Shina la Wakereketwa wa Noah Saccos, katika Stendi Kuu ya…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

ARUSHA: Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi, amewataka Watanzania kuendelea kulinda uhuru, amani na utulivu wa nchi kwa kupinga hadharani watu wanaohamasisha chokochoko na vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa taifa.

Kihongosi ameeleza hayo leo Juni 6,2026 alipotembelea na kuzindua Shina la Wakereketwa wa Noah Saccos, katika Stendi Kuu ya Mabasi Arusha mkoani humo, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake Kanda ya Kaskazini.

Akizungumza katika uzinduzi huo Kihongosi amesema Tanzania imejengwa juu ya misingi ya umoja, mshikamano na amani iliyopatikana kwa juhudi za waasisi wa taifa, hivyo wananchi wanapaswa kuendelea kuithamini na kuilinda.

“Hakuna jambo baya kama kuwa mtumwa ndani ya mataifa ya watu. Uhuru tulionao leo hapa, tulinde na wale wanaohamasisha chokochoko tuwapinge hadharani,” amesema.

Kihongosi amewataka wananchi kutokubali kutumiwa na wanasiasa wanaowashawishi kushiriki vitendo vinavyoweza kuhatarisha maisha yao na usalama wa taifa, akieleza kuwa mara nyingi madhara huwapata waliotangulizwa mbele huku waliohamasisha wakibaki salama.

Amesema baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiwatumia vijana kutekeleza ajenda zao bila kuzingatia athari zinazoweza kuwakumba, jambo ambalo linapaswa kukemewa na kukataliwa na jamii.

“Usitumike na wanasiasa kuhatarisha uhai wako, awatakusaidia, haki ya Mungu nawaambia leo, hata waliopata madhara wametelekezwa na hao wanasiasa waliowatuma,” amesema.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports