AAGIZA MAMLAKA KUTATUA KERO YA MAJI SAME – Habari Mpya

Asisitiza Tsh Trilioni 1.2 zimewekezwa Kilimanjaro, sasa ni zamu ya mfumo wa Usambazaji. MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Baraa, Stephen Wasira, ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Same (SAUWASA) kuhakikisha inatatua kwa haraka changamoto ya upatikanaji maji inayowakabili wananchi wa mji wa Same. Wasira alitoa agizo hilo leo Juni 8,…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

Asisitiza Tsh Trilioni 1.2 zimewekezwa Kilimanjaro, sasa ni zamu ya mfumo wa Usambazaji.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Baraa, Stephen Wasira, ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Same (SAUWASA) kuhakikisha inatatua kwa haraka changamoto ya upatikanaji maji inayowakabili wananchi wa mji wa Same.

Wasira alitoa agizo hilo leo Juni 8, 2026 alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM wa Shina Namba 9, Tawi la Same, Kata ya Same, wilayani Same mkoani Kilimanjaro.

Akijibu malalamiko ya wananchi kuhusu ukosefu wa maji, alisema haikubaliki kwa wakazi wa Same kuendelea kukosa huduma hiyo muhimu wakati maji yanapatikana kwa wingi kupitia miradi iliyotekelezwa na serikali.

“Ninaiagiza SAUWASA kuhakikisha wananchi wa Same wanapata maji. Haiwezekani watu wa Same waendelee kuyasikia au kuyaona maji bila kuyapata kwa matumizi yao ya kila siku, mfumo wa usambazaji uharakishwe ili wananchi wanufaike na huduma hiyo muhimu,” alisema Wasira.

Alibainisha kuwa, serikali imewekeza fedha nyingi kutekeleza mradi wa maji wa Same–Mwanga–Korogwe, hivyo hakuna sababu ya wananchi kuendelea kukosa huduma hiyo kutokana na changamoto za usambazaji.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports