Wadau watoa maoni urasimu sekta binafsi

DAR ES SALAAM: Mmoja wa wawekezaji katika sekta ya afya nchini Dk.Mahmood Mringo, ameishauri Serikali kufanya mageuzi makubwa ya kisera ili kunusuru sekta binafsi, akilalamikia utitiri wa kodi, mlolongo wa mamlaka za udhibiti, na riba kubwa za benki zinazokwamisha uwekezaji. Mringo aliwasilisha malalamiko hayo mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia (PPP Centre), David…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

DAR ES SALAAM: Mmoja wa wawekezaji katika sekta ya afya nchini Dk.Mahmood Mringo, ameishauri Serikali kufanya mageuzi makubwa ya kisera ili kunusuru sekta binafsi, akilalamikia utitiri wa kodi, mlolongo wa mamlaka za udhibiti, na riba kubwa za benki zinazokwamisha uwekezaji.

Mringo aliwasilisha malalamiko hayo mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia (PPP Centre), David Kafulila, wakati wa Kongamano la Kitaifa la PPP katika Sekta ya Afya lililofanyika katika Chuo Kikuu cha MUHAS.

Akiwasilisha kilio hicho, Mringo alimtaka Kafulila kufanyia kazi changamoto zao ili kutekeleza programu ya PPP katika sekta ya afya.

Pia kutatua changamoto zao ametaka kupunguza gharama za matibabu kwa wananchi, Mringo aliishauri Serikali kuanzisha utaratibu wa kutoa dhamana kwa wawekezaji wa afya ili wapate mikopo yenye riba nafuu.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports