BAJETI KUU, SERIKALI YAMWAGIWA MABILIONI KUKABILI MABADILIKO YA TABIANCHI – Habari Mpya

DOLA MIL 320 KUBORESHA MIUNDOMBINU ILIYOHARIBIKA KWA MABADILIKO YA TABIANCHI  Serikali imesema imepokea jumla ya dola za Marekani milioni 320 katika kipindi cha mwaka 2024/25 hadi 2025/26 ili kuboresha na kurejesha miundombinu muhimu iliyoharibika kutokana na mabadiliko ya tabianchi.  Pia, kwa kuzingatia hilo imesema itaendelea kuhakikisha kuwa masuala ya mabadiliko ya tabianchi ambayo Ofisi ya…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

DOLA MIL 320 KUBORESHA MIUNDOMBINU ILIYOHARIBIKA KWA MABADILIKO YA TABIANCHI 

Serikali imesema imepokea jumla ya dola za Marekani milioni 320 katika kipindi cha mwaka 2024/25 hadi 2025/26 ili kuboresha na kurejesha miundombinu muhimu iliyoharibika kutokana na mabadiliko ya tabianchi. 

Pia, kwa kuzingatia hilo imesema itaendelea kuhakikisha kuwa masuala ya mabadiliko ya tabianchi ambayo Ofisi ya Makamu wa Rais inasimamia yanazingatiwa kikamilifu katika mipango na bajeti. 

Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 bungeni jijini Dodoma Juni 11, 2026. 

Alisema athari za mabadiliko ya tabianchi zinaikumba Tanzania, hali inayoathiri sekta muhimu za uchumi hususan kilimo, maji, afya, uchukuzi na nishati hivyo Serikali imechukua hatua mbalimbali kukabiliana nazo. 

Katika kukabiliana nazo, Balozi Omar alisema kuwa Serikali imeanzisha matumizi ya utaratibu wa dharura chini ya Benki ya Dunia kwa ajili ya kukabiliana na athari za majanga yanayotokana na changamoto hizo. 

Kwa upande mwingine, alisema Serikali itaendelea kutoa motisha katika matumizi ya nishati safi ikiwemo ujenzi wa miundombinu wezeshi kwa ajili ya matumizi katika shughuli mbalimbali ikiwemo kupikia, viwandani pamoja na usafiri na usafirishaji. 

Balozi Omar alifafanua kuwa lengo la kutoa motisha hiyo ni kuhakikisha uwepo wa nishati salama na endelevu, kuokoa muda, kupunguza gharama pamoja na athari za kimazingira na kiafya kwa watumiaji. 

Hatua hiyo itachangia katika kuhifadhi mazingira kwa wananchi na taasisi kutumia nishati safi kupikia na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa yanayotokana na ukataji wa miti. 

Aidha, alisema pamoja na Mikakati mbalimbali Serikali itaendelea pia kutekeleza Mpango Kabambe wa Taifa wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (2022-2032), Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati safi ya Kupikia (2024–2034).

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports