Kadogosa: Biashara ndogondogo zahitaji mazingira wezeshi

MBUNGE wa Bariadi Vijijini, Masanja Kadogosa, amesema biashara ndogondogo zinapaswa kuwekewa mikakati madhubuti na mazingira rafiki ili ziweze kustawi na kutoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa. Akichangia mjadala wa Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2025, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa 2026/27 pamoja na Bajeti ya Serikali ya mwaka 2026/27,…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

MBUNGE wa Bariadi Vijijini, Masanja Kadogosa, amesema biashara ndogondogo zinapaswa kuwekewa mikakati madhubuti na mazingira rafiki ili ziweze kustawi na kutoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa.

Akichangia mjadala wa Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2025, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa 2026/27 pamoja na Bajeti ya Serikali ya mwaka 2026/27, Kadogosa amesema uamuzi wa kuziondolea kodi biashara ndogondogo katika mwaka wao wa kwanza wa uendeshaji ni hatua chanya itakayozisaidia kuanza na kukua. SOMA: Neema biashara za wananchi

Hata hivyo, amesisitiza kuwa mafanikio ya hatua hiyo yatategemea uwepo wa sera thabiti na mifumo wezeshi itakayowapa wafanyabiashara hao mazingira bora ya kujiimarisha. “Ni jambo zuri sana, lakini tunatakiwa kuwa na sera za ndani na lazima kuziwekea mazingira ili zistawi na zisimame,” amesema.

Kadogosa amesema mataifa mengi yaliyopiga hatua kiuchumi yamewekeza katika kukuza biashara ndogondogo na za kati (SMEs), ambazo zimekuwa chanzo kikubwa cha ajira na uzalishaji. Aidha, ameipongeza Bajeti ya Serikali ya mwaka 2026/27, akieleza kuwa itaweka msingi muhimu wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports