Maadhimisho ya Kiswahili Duniani  kufanyika Julai nchini Burundi

Zanzibar. Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (Kakama) imetangaza maadhimisho ya Siku Kiswahili kuwakutanisha wananchi kutoka mataifa manane ya Afrika Mashariki mjini Bujumbura, Burundi. Akizungumza leo Juni 19,2026 na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali, Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili (Kakama), Dk Caroline Asiimwe amesema maadhimisho hayo yatafanyika kuanzia Julai 5-7, 2026.…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

Zanzibar. Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (Kakama) imetangaza maadhimisho ya Siku Kiswahili kuwakutanisha wananchi kutoka mataifa manane ya Afrika Mashariki mjini Bujumbura, Burundi.

Akizungumza leo Juni 19,2026 na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali, Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili (Kakama), Dk Caroline Asiimwe amesema maadhimisho hayo yatafanyika kuanzia Julai 5-7, 2026.

Amesema maadhimisho ya Kiswahili yatatanguliwa na Kongamano la Tatu ka Kakama na kufuatiwa na Siku ya Kiswahili Duniani Julai 7.

Amesema maadhimisho ya kongamano la Kakama yamekuwa yakifanyika kila baada ya miaka miwili na kutoa fursa kwa kila nchi wanachama.

Amesisitiza kwamba maadhimisho hayo yamewezesha wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kunufaika na fursa mbalimbali kupitia Kiswahili.

Aidha lugha ya Kiswahili imetajwa kufikia hadhi ya kimataifa kiwango cha kuwezesha kuwa na mchango wa maendeleo katika nchi wanachama Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amesema lugha ya Kiswahili inaweza kumwezesha mwekezaji kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo katika nchi husika kutokana na kutumika na takribani nchi nane wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambazo lugha ya Kiswahili inatambulika rasmi na kuzungumzwa.

Dk Asiimwe amesema lugha ya Kiswahili inamwezesha hata mjasiriamali na mfanyabiashara aliyepo kijijini kuamua kuchagua lugha atakayo kupitia akili unde ili kumwezesha kuwasiliana kikamilifu.

Amesema kutokana na maendeleo ya teknolojia, yamewasukuma katika maadhimisho ya Kiswahili mwaka huu kubeba mjadala wa akili unde na wingi lugha.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports