iTRUST YAFIKIA THAMANI YA BIL.176, YAWAKUTANISHA WAWEKEZAJI KATIKA MKUTANO MKUU – Habari Mpya

Dar es Salaam, Tanzania – Juni 20, 2026 Kampuni ya iTrust Finance Limited imetangaza mafanikio makubwa baada ya thamani ya mali inayosimamiwa kufikia zaidi ya Shilingi bilioni 176, hatua inayotajwa kuwa ni miongoni mwa mafanikio makubwa katika historia ya kampuni hiyo ya uwekezaji. Kwa mujibu wa taarifa ya fedha zilizokaguliwa kwa mwaka uliomalizika tarehe 31…

admin Avatar

by

2 minutes

Read Time

Dar es Salaam, Tanzania – Juni 20, 2026

Kampuni ya iTrust Finance Limited imetangaza mafanikio makubwa baada ya thamani ya mali inayosimamiwa kufikia zaidi ya Shilingi bilioni 176, hatua inayotajwa kuwa ni miongoni mwa mafanikio makubwa katika historia ya kampuni hiyo ya uwekezaji.

Kwa mujibu wa taarifa ya fedha zilizokaguliwa kwa mwaka uliomalizika tarehe 31 Desemba 2025, mifuko mitano ya uwekezaji inayosimamiwa na iTrust imefikia thamani hiyo kupitia mifuko ya iCASH Fund, iSAVE Fund, iINCOME Fund, iGROWTH Fund na IMAAN Fund.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa thamani ya mali inayosimamiwa kwa kila mfuko ni pamoja na iCASH Fund Shilingi milioni 36,045, iSAVE Fund Shilingi milioni 10,656, iINCOME Fund Shilingi milioni 16,352, iGROWTH Fund Shilingi milioni 97,999 na IMAAN Fund Shilingi milioni 14,915.

Mafanikio hayo yamewasilishwa wakati wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wanahisa (Annual General Meeting – AGM) wa mifuko hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam Juni 20, 2026, ukiwaleta pamoja wawekezaji kwa ajili ya kupitia utendaji wa mifuko yao na kujadili hatua mbalimbali za maendeleo ya uwekezaji.

Kupitia mkutano huo, wawekezaji walipata fursa ya kupokea taarifa kutoka kwa Mdhamini (Trustee), wakaguzi wa hesabu wa nje, pamoja na kuuliza maswali kuhusu mwenendo wa mifuko hiyo na mipango ya baadaye.

“Mkutanohu umefanyika ikiwa ni sehemu ya kuendeleza misingi ya uwazi, uwajibikaji na ushirikishwaji wa wawekezaji,” ilieleza taarifa hiyo, huku ikibainisha kuwa hatua hiyo inalenga kuimarisha utawala bora na kuongeza ufanisi wa uendeshaji wa mifuko.

Aidha, wawekezaji walijadili mapendekezo mbalimbali ya marekebisho kwenye Hati za Dhamana (Trust Deeds) zinazosimamia mifuko hiyo kwa lengo la kuboresha utendaji, kupanua fursa za uwekezaji na kuhakikisha mifuko inaendelea kuendana na mabadiliko ya soko.

Miongoni mwa mapendekezo yaliyowasilishwa ni kuruhusu iGROWTH Fund kuwekeza katika Exchange Traded Funds (ETFs), hatua inayolenga kuongeza wigo wa uwekezaji na kuwapatia wawekezaji fursa zaidi katika masoko ya fedha.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa maboresho hayo ni sehemu ya mkakati wa iTrust Finance Limited kuendelea kuboresha bidhaa zake za uwekezaji huku ikizingatia viwango vya juu vya usimamizi, ulinzi wa wawekezaji na kanuni za masoko ya fedha.

Mbali na mafanikio hayo, iTrust imeendelea kuwekeza katika teknolojia baada ya kuzindua iTrust App, mfumo wa kidijitali unaowawezesha wawekezaji kufuatilia uwekezaji wao, kupata taarifa za soko kwa wakati halisi na kufanya maamuzi ya kifedha kwa urahisi zaidi.

Kampuni hiyo imeeleza kuwa ukuaji wa mifuko yake unaonesha kuongezeka kwa imani ya Watanzania katika mifumo ya uwekezaji wa pamoja (Unit Trust Schemes) kama njia ya kujenga utajiri wa muda mrefu na kufikia malengo ya kifedha.

iTrust Finance Limited ni kampuni yenye leseni kutoka Benki Kuu ya Tanzania na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana kwa ajili ya kutoa huduma za usimamizi wa uwekezaji, udalali wa hisa na shughuli nyingine za kifedha zinazohusiana na uwekezaji.

Kupitia ukuaji wa mali inayosimamiwa, ubunifu wa bidhaa na matumizi ya teknolojia, iTrust imeeleza dhamira yake ya kuendelea kuwawezesha Watanzania na taasisi kujenga utajiri wa muda mrefu kwa njia salama, rahisi na yenye uwazi.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports