Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah, amewasili katika Makao Makuu ya Nchi jijini Dodoma, kuendele na ziara yake ya Kitaifa ya siku tatu kuanzia Juni 19 hadi 21, 2026. Alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Dodoma alipokelewa na Waziri wa Nchi. Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.
Akiwa jijini Dodoma Mhe. Dkt. Netumbo atatembelea iliyokuwa Kambi ya Wapigania Uhuru wa Namibia iliyopo Wilayani Kongwa na Kiwanja cha Ubalozi wa Namibia kilichopo Mji wa Serikali, Mtumba.












