NMB Foundation, Tacaids waungana kumkomboa msichana dhidi ya Ukimwi

Dodoma. Taasisi ya NMB Foundation na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (Tacaids) zimesaini makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa Timiza Malengo unaolenga kuwafikia zaidi ya wasichana na wanawake 10,000 katika halmashauri 36 za mikoa kumi nchini. Makubaliano hayo yaliyosainiwa jijini Dodoma yanatajwa kuwa sehemu ya mkakati wa kuunganisha mapambano dhidi ya Ukimwi na uwezeshaji wa…

admin Avatar

by

2 minutes

Read Time

Dodoma. Taasisi ya NMB Foundation na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (Tacaids) zimesaini makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa Timiza Malengo unaolenga kuwafikia zaidi ya wasichana na wanawake 10,000 katika halmashauri 36 za mikoa kumi nchini.

Makubaliano hayo yaliyosainiwa jijini Dodoma yanatajwa kuwa sehemu ya mkakati wa kuunganisha mapambano dhidi ya Ukimwi na uwezeshaji wa kiuchumi, kwa lengo la kupunguza maambukizi mapya hasa kwa kundi la vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 ambalo bado linaelezwa kuwa katika hatari zaidi.

Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo, Meneja Mkuu wa NMB Foundation, Nelson Karumuna amesema mradi huo utawajengea uwezo wasichana na wanawake katika maeneo ya elimu ya fedha, ujasiriamali, stadi za maisha na huduma za kinga dhidi ya VVU.

Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk Adam Mrisho (kulia, akibadilishana hati ya makubaliano na Meneja Mkuu wa NMB Foundation, Nelson Karumuna, mara baada ya kusaini makubaliano ya utekelezaji wa pamoja wa Mradi wa TIMIZA Malengo kati ya TACAIDS na NMB Foundation, jijini Dodoma.

“Kupitia makubaliano haya, tunakwenda kuwajengea uwezo wasichana na wanawake zaidi ya 10,000 katika halmashauri 36 ndani ya mikoa 10. Lengo ni kuwawezesha kukuza biashara zao, kupata elimu ya fedha, stadi za maisha na huduma za kinga kwa sababu afya na uchumi lazima viende pamoja,” amesema Karumuna.

Ameongeza kuwa mtandao mpana wa NMB Foundation kupitia zaidi ya mawakala 73,000 nchini utasaidia kufikisha huduma za kifedha na elimu ya uwezeshaji hadi ngazi ya jamii, hususan maeneo ya pembezoni.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tacaids, Dk Adam Mrisho amesema ushirikiano huo unalenga kujenga kizazi chenye afya, maarifa na uwezo wa kiuchumi, akisisitiza uwezeshaji wa wasichana ni nyenzo muhimu ya kupunguza maambukizi mapya ya VVU nchini.

“Afya ya vijana ndiyo uchumi wa Taifa. Tunapowawezesha wasichana kwa elimu, stadi za maisha na fursa za kiuchumi, tunajenga kesho imara zaidi na kupunguza mazingira hatarishi yanayoweza kuongeza maambukizi,” amesema Dk Mrisho.

Amebainisha kuwa Tanzania imepiga hatua katika kupunguza maambukizi mapya ya VVU kutoka asilimia 0.27 hadi 0.17, lakini akasisitiza kuwa mafanikio hayo yanahitaji kuendelezwa kupitia ushirikiano wa sekta mbalimbali.

Akishungumza kwenye hafla hiyo,  Mwanasheria wa Tacaids, Miraj Mambo amesema ushirikiano huo na NMB Foundation unalenga kuimarisha utekelezaji wa Mradi wa Timiza Malengo kwa kuzingatia maeneo ya kinga, elimu ya afya, ujasiriamali na ushirikishwaji wa jamii.

Kwa ujumla, makubaliano hayo yanatarajiwa kuimarisha juhudi za kitaifa za mapambano dhidi ya Ukimwi huku yakijenga msingi wa kuwawezesha wasichana na wanawake kiuchumi na kijamii kupunguza hatari ya maambukizi mapya ya VVU nchini.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports