Mauaji mwekezaji wa China Chalamila amuomba radhi Rais Samia

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amemuomba radhi Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia kuuawa kwa raia wa China ambaye alikuwa mwekezaji na mmiliki wa kiwanda cha kuchakata chupa za plastiki cha XIL LI, Bhaozang Ge (50). Mmiliki huyo raia wa China aliuawa na watu wanaodaiwa ni walinzi binafsi wa…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amemuomba radhi Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia kuuawa kwa raia wa China ambaye alikuwa mwekezaji na mmiliki wa kiwanda cha kuchakata chupa za plastiki cha XIL LI, Bhaozang Ge (50).

Mmiliki huyo raia wa China aliuawa na watu wanaodaiwa ni walinzi binafsi wa kiwanda hicho kilichopo Mabibo, Dar es Salaam usiku wa kuamkia Jumamosi ya Mei 16, 2026.

Mei 24, 2026, mwili wa mwekezaji huyo ulichomwa moto katika eneo maalumu la Makumbusho ya Taifa na Mei 27, 2026 majivu yake yalisafirishwa na wanafamilia kwenda nchini China kwa ajili ya mazishi.

Leo Alhamisi, Mei 28, 2026 mbele ya Rais Samia katika hafla ya kuhitimisha mafunzo ya maofisa na wakaguzi wasaidizi wa polisi, Chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es Salaam, Chalamila amegusia mauaji ya mwekezaji huyo.

“Mheshimiwa Rais utuwie radhi, wiki iliyopita tulipata dosari kama mkoa baada ya mmoja wa wawekezaji kutoka jamii ya Wachina kuuawa katika eneo la uwekezaji,”amesema na kuongeza.

“Tukio hilo tunafahamu linaweza kusababisha kasoro katika diplomasia na uhusiano wake, lakini naomba kukuthibitishia chini ya viongozi wetu kwa Mkoa wa Dar es Salaam wahusika watakamatwa,”amesema.

“Nataka nikudhibitishie Mheshimiwa Rais, watu wote waliohusika watakamatwa,” amesema.

Chalamila amemweleza Rais Samia kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi yanapotokea mambo ya namna hiyo jamii kushirikiana na Jeshi la Polisi na si busara kuanza kuwanyooshea vidole watu wasiohusika moja kwa moja na tukio hilo.

Amesema Mkoa wa Dar es Salaam ambao ndio mkubwa kidiplomasia, kiuchumi na demografia ya watu, upo salama leo na hata baadaye.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports