Hemed: Hatuwezi kusonga mbele bila kushirikisha sekta binafsi

Unguja. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amesema maendeleo ya kweli hayawezi kupatikana bila ushirikiano, hivyo Serikali inahitaji kushikamana na sekta binafsi kujenga uchumi imara. Hemed ametoa kauli hiyo leo Jumapili Mei 31, 2026 Fumba baada ya matembezi ya hiari ya kilometa tano yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (Zipa).…

admin Avatar

by

3 minutes

Read Time

Unguja. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amesema maendeleo ya kweli hayawezi kupatikana bila ushirikiano, hivyo Serikali inahitaji kushikamana na sekta binafsi kujenga uchumi imara.

Hemed ametoa kauli hiyo leo Jumapili Mei 31, 2026 Fumba baada ya matembezi ya hiari ya kilometa tano yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (Zipa).

Matembezi hayo ni sehemu ya maandalizi ya mkutano mkubwa wa uwekezaji unaojulikana kama Zanzibar Investiment Summit mwaka 2026 unaotarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia Juni 3 hadi 5 mwaka huu na kuwakutanisha zaidi ya wawekezaji 500 kutoka mataifa mbalimbali kisiwani hapa.

Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inaendelea kuweka mazingira mazuri na rafiki kwa wawekezaji kuhakikisha uwekezaji unaongeza ajira kwa vijana, unakuza uchumi na maendeleo ya moja kwa moja kwa wananchi.

“Maendeleo ya kweli hayawezi kupatikana bila ushirikiano, tunahitaji kuendelea kushikamana kama jamii, Serikali, sekta binafsi, wadau wa maendeleo ili kufanikisha malengo ya kujenga Zanzibar yenye uchumi imara na wananchi wenye afya njema na ustawi,” amesema Hemed.

Katika siku hizo tatu za mkutano huo, amesema wawekezaji hao watapata fursa za kutembelea na kuona miradi mbalimbali ya maendeleo ya uwekezaji.

“Itatoa fursa ya kipekee kwa wawekezaji kujionea mazingira mazuri za uwekezaji na hatua kubwa zinazochukuliwa na Serikali katika kukuza uchumi wa taifa,” amesema.

Hemed amesema mkutano huo utatoa pia fursa kwa Diaspora kujadili namna bora kwao kuweza kushiriki katika uwekezaji wa maendeleo ya Zanzibar kupitia mitaji, utaalamu na  ushirikiano wa kiuchumi.

Kupitia mkutano huo, Zanzibar itaendelea kujitangaza kama kitovu cha uwekezaji na biashara katika ukanda huu hususani katika maeneo ya vipaumbele ikiwamo utalii, miundombinu, uchumi wa buluu, tekenolojia na huduma za kijamii.

Pia, mkutano huo utajumuisha mipango mbalimbali ikiwamo investment Master Classes zitakazojadilia mada muhimu zitakazohusu namna ya kuandaa miradi katika masoko yanayochipukia.

Kingine kitakachojadiliwa katika mkutano huo, ni mbinu za kupunguza vihatarishi vya uwekezaji, pamoja na fursa za uwekezaji zenye faida kubwa katika sekta ya kilimo, biashara, viwanda, usafirishaji na ugavi.

Kadhalika kutakuwa na mijadala ya kitaalamu itakayowakutanisha wadau wakubwa wa maendeleo, wawekezaji, taasisi za kifedha na viongozi wa sekta za Serikali na binafsi kujadili mustakabali wa uchumi wa Zanzibar ikiwamo kuhusu nini kitakachobeba hatua inayofuata ya ukuaji wa uchumi wa Zanzibar.

Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushiriki katika shughuli za kijamii, michezo na maendeleo zinazoimarisha mshikamano wao na kuleta manufaa.

Naye Waziri wa Kazi na Uwekezaji, Sharrif Ali Sharrif amesema programu hizo zinazofanyika zinatokana na jukwaa kubwa la uwekezaji ambalo linatarajia kuwa na matokeo chanya kwa visiwa vya Zanzibar.

“Hapa tulipo Fumba imetengenezwa mpango mkakati wa miji ambapo kwa sasa tutakuwa na miji mikuu miwili: Stone Town na huu wa Fumba, ” amesema Sharrif

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (Zipa), Saad Saleh Mohamed amesema mpaka sasa maandalizi ya mkutano huo yapo tayari na hiyo ni shamrashamra ambazo ni ishara ya maendeleo

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mohamed Ali Abdallah amesema katika kujenga mji huo na uwanja wa Afcon unaojengwa katika eneo hilo, utaweka historia sio Zanzibar pekee bali Afrika Mashariki.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports