Mambo sita yanayonogesha uhusiano | Mwananchi

Dar es Salaam. Wengi wetu tunapitia changamoto nyingi katika ndoa au uhusiano wetu. Wapo ambao hawapendi hali wanazopitia lakini hawajui chanzo ni nini; wengine wanajua tatizo lilipo, lakini hawajui namna ya “kuchomoka,” jambo linaloongeza msongo wa mawazo. Ukweli ni kwamba kuna mambo ya msingi ambayo wengi hawayajui, na wale wanaoyajua mara nyingi hawayafanyii kazi, hivyo…

admin Avatar

by

3 minutes

Read Time

Dar es Salaam. Wengi wetu tunapitia changamoto nyingi katika ndoa au uhusiano wetu.

Wapo ambao hawapendi hali wanazopitia lakini hawajui chanzo ni nini; wengine wanajua tatizo lilipo, lakini hawajui namna ya “kuchomoka,” jambo linaloongeza msongo wa mawazo.

Ukweli ni kwamba kuna mambo ya msingi ambayo wengi hawayajui, na wale wanaoyajua mara nyingi hawayafanyii kazi, hivyo kusababisha misuguano isiyoisha.

 Makala hii inakuletea mambo sita muhimu yatakayokusaidia kuboresha na kuyafurahia uhusiano wako.

Sababu kubwa inayofanya watu washindwe kuona mabadiliko kwa wapenzi wao ni kuanza vibaya safari ya mabadiliko.

 Kabla ya kumlalamikia mwenzako kuhusu upungufu wake, jiangalie wewe kwanza. Je, kuna mambo mpenzi wako anayalalamikia kwako? Jitahidi kuyabadili hayo kwanza.

Ukianza kwa kujirekebisha, unamuandaa mwenzako kisaikolojia kupokea mwito wa yeye pia kubadilika. Kumlazimisha mabadiliko wakati wewe bado ni “yule yule” huleta upinzani badala ya maelewano.

 Epuka mtazamo wa “Nitalipiza”

Watu wengi huishi kwa kanuni ya: “Nitabadilika kama yeye akibadilika” au “Akifanya hivi, na mimi nitafanya vile.” Tuwe wa kweli; dhana hii ya mashindano haijawahi kufanikiwa.

Uhusiano si uwanja wa vita wa kulinganishana makosa. Amua kubadilisha mtazamo kwa kutafuta kuwa bora wewe kwanza, bila kusubiri kusukumwa.

 Tafuta uhuru wa ndani kwa uwazi

Unaweza kufanikiwa kuficha makosa yako, lakini siri hizo zitakunyima amani ya ndani. Kujihisi mwenye hatia wakati wote si hali njema kwa afya yako ya akili. Unapoamua kukiri makosa yako kwa uwazi mbele ya mpenzi wako, unajifungua kutoka kwenye utumwa wa uovu.

Uwazi huu hupanua uwezekano wa kuleta mabadiliko ya kweli na ya kudumu katika uhusiano yenu.

Toba kwa Mungu isiondoe msamaha kwa mwenza

Wengi wetu ni watu wa imani. Tunapokosea, tunakimbilia kuomba msamaha kwa Mungu—hilo ni jambo jema. Lakini katika uhusiano wa kibinadamu, hatua hiyo haitoshi. Ni lazima ukiri kosa na kuomba radhi kwa mpenzi wako uliyemuumiza.

 Usahihishaji wa mambo kwa Muumba uende sambamba na usahihishaji wa mambo kwa mwanadamu uliyenaye karibu.

Ni kweli kuwa makosa mengine hayawezi kufutika kabisa hata baada ya kuomba msamaha.

Hata hivyo, lengo la kukiri si kufuta yaliyopita, bali ni kuonyesha kuwa unajutia maumivu uliyosababisha. Unapokubali kuwa ulihusika na unajisikia vibaya kwa kumuumiza mwenzako, unajijengea uhalali wa kusamehewa na kuanza upya safari yenu kwa misingi ya kuaminiana.

 Tumia lugha ya kutia moyo na kusifu

Miongoni mwa lugha za mapenzi zenye nguvu zaidi ni maneno ya faraja na pongezi. Jiulize:

Lini mara ya mwisho umemwambia mpenzi wako amependeza?

Lini umempongeza kwa jambo dogo alilofanya vizuri?

Lini umemwambia kuwa yeye ni wa muhimu sana maishani mwako?

Wengi hufikiri kusema “nakupenda” siku ya harusi inatosha kwa maisha yote. Hiyo si kweli! Kama vile bosi asivyoweza kukunyima pongezi leo kwa sababu alikupongeza mwaka juzi, ndivyo na mpenzi wako anavyohitaji kusikia maneno matamu kila siku.

 Lugha ya sifa na kutia moyo huiinua nafsi, wakati lawama, kejeli, na matusi huua upendo moyoni.

Kumbuka uhusiano bora hauji kwa bahati mbaya; hujengwa kwa makusudi. Anza leo kufanyia kazi mambo haya, nawe utaona matunda ya kiu yako ya kuwa na uhusiano wenye furaha na amani.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports