Mahakama kusikiliza tena maombi ya Lissu Juni 2

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam imewapa siku saba wajibu maombi katika shauri la Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, kujibu maombi yake huku ikipanga kusikiliza shauri hilo Juni 2, 2026. Lissu, ambaye yuko mahabusu kutokana na kesi ya uhaini, ameomba kujumuishwa katika kesi ya madai ya…

admin Avatar

by

3 minutes

Read Time

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam imewapa siku saba wajibu maombi katika shauri la Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, kujibu maombi yake huku ikipanga kusikiliza shauri hilo Juni 2, 2026.

Lissu, ambaye yuko mahabusu kutokana na kesi ya uhaini, ameomba kujumuishwa katika kesi ya madai ya mgawanyo usio sawa wa rasilimali ndani ya chama hicho kati ya Bara na Zanzibar.

Kesi hiyo ya madai namba 8323 ya mwaka 2025 imefunguliwa na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa Chadema, Said Issa Mohamed, pamoja na wajumbe wawili wa Bodi ya Wadhamini wa Chadema kutoka Zanzibar, Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu (marehemu kwa sasa).

Wadaiwa ni Bodi ya Wadhamini Waliosajiliwa wa Chadema na Katibu Mkuu wa chama hicho.

Kutokana na kesi hiyo, Lissu amefungua maombi akiomba kuunganishwa katika shauri hilo kwa wadhifa wake wa Mwenyekiti wa Chadema Taifa, akidai ana masilahi ndani ya kesi hiyo.

Wajibu maombi wa kwanza hadi wa tatu ni wadai wa kesi ya msingi, huku Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa Chadema wakiwa wajibu maombi wa nne na wa tano.

Shauri hilo la maombi mchanganyiko namba 12194/2026 limetajwa leo Jumatatu Mei 25, 2026. Wajibu maombi wa kwanza hadi wa tatu kupitia wakili wao, Shabani Marijani, waliieleza mahakama kuwa hawakuwa wamepewa nyaraka za shauri hilo.

Wakili Marijani amesema walipata taarifa za kuwepo kwa shauri hilo jana kupitia mitandao ya kijamii na baadaye kuliona kwenye mfumo wa mahakama.

“Kwa hiyo tunaomba siku 14 tuweze kuwasilisha counter affidavit kwa mujibu wa sheria,” amesema Wakili Marijani.

Hata hivyo, Lissu pamoja na wajibu maombi wa nne na wa tano kupitia mawakili wao wakiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Dk Rugemeleza Nshala, walipinga ombi hilo na kuomba mahakama itoe siku chache ili shauri lisikilizwe haraka.

Jaji David Ngunyale alikubaliana na hoja hiyo na kutoa siku saba kwa wajibu maombi kuwasilisha viapo kinzani kabla ya Mei 31, 2026.

“Kwa hiyo shauri hili litasikilizwa Juni 2, 2026,” amesema Jaji Ngunyale.

Hata hivyo, usikilizwaji wa shauri hilo utategemea uamuzi wa pingamizi lililowekwa katika kesi ya msingi, ambapo wadaiwa wanadai kesi hiyo ni batili kwa kutokubainisha muda wa kuanza kwa madai hayo.

Uamuzi wa pingamizi hilo unatarajiwa kutolewa Mei 28, 2026 na ndio utaamua hatima ya kesi hiyo.

Iwapo pingamizi litakubaliwa, kesi ya msingi itaondolewa mahakamani na maombi ya Lissu nayo yatakufa moja kwa moja. Lakini kama litakataliwa, kesi ya msingi pamoja na maombi ya Lissu vitaendelea kusikilizwa.

Hii ni mara ya pili kwa Lissu kufungua maombi hayo. Awali aliwasilisha maombi kwa jina lake binafsi akidai ana maslahi makubwa katika kesi hiyo kwa kuwa ni mwenyekiti wa chama.

Katika uamuzi uliotolewa Aprili 30, 2026 na kusomwa na Naibu Msajili, Hussein Mushi, Jaji Hamidu Mwanga alimkatalia Lissu kuunganishwa katika kesi hiyo akisema hakuonyesha maslahi ya moja kwa moja yanayompa sifa ya kujumuishwa katika shauri hilo.

Jaji Mwanga alisema masilahi aliyoyaonyesha yalikuwa ya kiuwakilishi kutokana na nafasi ya uenyekiti anayoshikilia, nafasi ambayo inaweza kushikiliwa na mtu mwingine wakati wowote.

Baada ya uamuzi huo, Lissu amerejea tena mahakamani safari hii akitumia wadhifa wake wa Mwenyekiti wa Chadema badala ya jina lake binafsi.

Katika kesi ya msingi, wadai wanadai kuna mgawanyo usio sawa wa mali na rasilimali za chama kati ya Zanzibar na Tanzania Bara, kinyume cha Sheria ya Vyama vya Siasa na Katiba ya Chadema.

Pia wanadai kuwepo kwa ubaguzi wa kidini na kijinsia pamoja na matamko yanayoweza kuvuruga Muungano wa Tanzania.Wadai wanaiomba mahakama itamke kuwa wadaiwa wamekiuka kifungu cha 6A(1), (2) na (5) cha Sheria ya Vyama vya Siasa na kuwa mgawanyo wa fedha, mali na rasilimali unaofanywa ni batili.

Aidha, wanaomba shughuli zote za kisiasa za chama hicho zisitishwe kwa muda hadi maagizo ya mahakama yatakapotekelezwa pamoja na zuio la matumizi ya mali na rasilimali za chama hadi matakwa ya sheria yatimizwe.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports